Tanzania House of Talent ‘THT,’ Amini Mwinyimkuu Mpili. Mshkaji alizaliwa 1986 katika Hospitali ya Mwananyamala Kinondoni jijini Dar es Salaam akiwa ni mtoto wa mwisho kati ya watoto saba wa mzee Mwinyimkuu.
Alianza safari ya masomo 1997 katika Shule ya Msingi Kinondoni na kuhitimu mwaka 2003. Kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wake hakuendelea na masomo ya sekondari.
Hata hivyo mwishoni mwa mwaka 2003 aliamua kusoma English Course mtaani kwao kwa ‘teacher’ mmoja aliyemtaja kwa jina la Chris kwa muda wa miezi sita kisha kujiingiza kwenye muziki.